“Msimu ulikuwa ni mrefu na mgumu. Nahitaji kwenda kupumzika sasa. Nina furaha tumeshinda mataji makubwa, la Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho. Naamini hata wazazi wangu mawinguni watakuwa wamefurahi kwa nilichofanya. Nataka kwenda kupumzika sasa nimeimisi familia yangu,”
Hii ni kauli ya kocha wa Yanga, Miguel Gamond baada ya kuiongoza timu hiyo kushinda fainali ya Shirikisho juzi kwa penalti 6-5 dhidi ya Azam FC.
Gamondi amefanuikiwa kuiongoza Yanga kushinda Kombe la Ligi Kuu 2023/24 pamoja na Kombe la Shirikisho.