UTARATIBU WA KUHAKIKI VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO KWA WAOMBAJI WA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2024/2025
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) wanafanya Uhakiki wa Vyeti vya Kuzaliwa na vyeti vya vifo (ikiwa muombaji amepoteza mzazi mmoja au wote) vya waombaji wanaotarajiwa kuomba mikopo ya masomo HESLB inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kwa mwaka 2024/2025. Maombi yote yanafanyika kwa njia ya mtandao pekee.
Waombaji wanaohakiki wanatakiwa kufuata maelezo yafuatayo:
1- Kila muombaji aingie katika mtandao kwa anuani: https://erita.rita.go.tz/auth ili kujisajili na kupata akaunti maalumu ambayo ataitumia kutuma nakala ya cheti kinachohakikiwa, namba ya uthibitisho wa malipo/ risiti (ambayo atatumiwa kwa ujumbe wa simu malipo yanapokamilika) na kupokea nakala ya cheti kilichohakikiwa.
HATUA ZA KUFANYA MAOMBI
MUHIMU
» Kila muombaji afungue akaunti binafsi ya uhakiki na atunze nywila (password) ya akaunti yake.
» Tuma kivuli cha cheti kinachosomeka vizuri na hakikisha namba ya ingizo (entry number) inasomeka
vizuri.
» Utapokea ujumbe wa kukiri kupokea nyaraka zako kwa maombi yaliyotumwa kikamilifu.
» Majibu ya uhakiki yatatumwa katika akaunti uliyofungua.
» Waombaji waliohakikiwa mwaka jana na vyeti vyao kuthibitishwa ni halali hawatakiwi kurudia uhakiki
Kwa maswali na maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia:
Simu: 0800117482 (bila malipo) / Barua pepe: Info@rita.go.tz
www.rita.go.tz | www.facebook.com/ritatanzania