Sifa na Vigezo Vya Kuomba Mkopo HESLB



Sifa za Kupata Mkopo HESLB. Sheria na Kanuni za Bodi ya Mikopo zinaainisha sifa na vigezo vya jumla kwa wanafunzi wanaohitaji mkopo baada ya kudahiliwa na vyuo vyenye ithibati.


Sifa za jumla kwa waombaji mkopo ni zifuatazo:


1. Awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 35 wakati wa kuomba mkopo;


2. Awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu ya juu yenye ithibati kikiwemo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania;


3. Awe ameomba mkopo kupitia mfumo wa maombi ya mkopo (OLAMS);


4. Asiwe na chanzo kingine kinachogharimia masomo yake ya elimu ya juu;


5. Kwa mwombaji aliyewahi kunufaika na mkopo wa HESLB, awe amerejesha angalau asilimia 25 ya fedha ya mkopo aliokuwa amekopeshwa awali;


6. Awe amehitimu elimu ya kidato cha sita (ACSEE) au stashahada (diploma) ndani ya miaka mitano iliyopita, kati ya mwaka 2019 hadi 2023.


ANGALIZO

Taarifa hii inalenga kutoa maelezo ya jumla ya awali ili kuwawezesha waombaji mkopo kujiandaa. Hivyo, tunapenda kusisitiza waombaji mkopo kuusoma na kuuzingatia Mwongozo utakaotolewa kila mwaka na bodi ya mkopo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Bottom Post Ad