Mwongozo (Guideline & Criteria) Utoaji Mikopo 2024/2025


Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Mwaka wa Masomo 2024/2025


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Mwaka wa Masomo 2023/2024’ wenye maelezo ya kina ya vigezo na utaratibu wa maombi unapatikana katika www.heslb.go.tz


Waombaji mikopo wanashauriwa kujiandaa kwa kuhakikisha yafuatayo:


i. Kuwa na akaunti ya benki yenye jina sawa na kwenye cheti chake cha kidato cha nne;


ii. Kuwa na namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake ambayo ataitumia akiwa chuoni;


iii. Kuhakiki cheti chake cha kuzaliwa kwa kufuata maelekezo ya RITA (Tanzania Bara) au ZCSRA (Zanzibar);


iv. Kuandaa nakala ya kitambulisho cha mdhamini wake; kinaweza kuwa kimoja kati ya NIDA, Kadi ya Mpiga Kura, Leseni ya Udereva, Pasi ya Kusafiria, au Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi;


v. Kuandaa picha ndogo za rangi (pass-port size) za mwombaji mkopo na mdhamini wake; na


vi. Kuandaa namba ya NIDA. Kama mwombaji hana kwa sasa, haitamzuia kufanya maombi ya mkopo.


Bodi ya Mikopo napenda kuwafahamisha waombaji mkopo watarajiwa kuwa watakuwa na muda wa kutosha wa siku 90 wa kuomba mkopo. 


“Miongozo hiyo inapatikana kwenye tovuti yetu ya Bodi ya Mikopo ya www.heslb.go.tz  toka Juni 01, 2024 na nawasihi waombaji mikopo kusoma na kuielewa miongozo hiyo kabla ya kuanza kufanya maombi ya mkopo, pamoja na kuzingatia muda uliopangwa wa kujaza maombi ya mkopo wa siku tisini (90), kuanzia Juni 01 hadi Agosti 31, 2024”, amesisitiza Dkt. Kiwia.


Bonyeza hapa ku download Mwongozo PDF

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Bottom Post Ad