Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda inaelezwa yupo mbioni kurejea Coastal Union kwa nia ya kwenda kuiongezea nguvu timu hiyo itakayoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/2025.
Mgunda anaenda kusaidiana na David Ouma na inadaiwa mazungumzo yapo mahali pazuri na muda wowote inaweza kutangazwa kurejea kwa Mgosi kwa Wagosi.