HENOCK INONGA ATIMUKIA FAR RABAT YA MOROCCO



Beki wa kati wa Simba, Henock Inonga anatajwa Kujiunga na FAR Rabat ya Morocco kwa kipindi cha miaka miwili (2)

Inaelezwa Inonga amesaini FAR Rabat, kipindi timu Taifa ya DR Congo ilipokuwa Rabat - Morocco.

Inonga hajatumika katika mechi kadhaa za mwishoni mwa msimu kwa kilichoelezwa kuwa majeruhi, japo taarifa nyingine zinasema ni ‘mgomo’ baridi aliokuwanao kutokana na kutuhumiwa tangu pambano la Dabi ya Kariakoo ambapo Simba ilichapwa 5-1 na ziliporudiana ikafungwa tena 2-1.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Bottom Post Ad